Ijumaa, 13 Januari 2017

Finally Mapinduzi Cup

Mapinduzi Fainali ni leo!!
Saa 2:15 usiku tukutane AzamONE na HD kushuhudia nani kuibuka kidedea???
Azam FC v Simba SC

Alhamisi, 12 Januari 2017

Tanzania yapangwa kundi jepesi Africon

Timu ya Taifa Tanzania imepangwa kundi L katika kufuzu michuano ya Africon 2019 huko Cameron, Tanzania imepangwa pamoja na timu ya Taifa Uganda ambao ni majirani zetu pamoja na Cape Verde visiwa hivi bila kuwasahau Lesotho

Simba Wajipange Finally #Mapinduzi_cup

Simba SC wajipange vyema mechi ya kesho dhidi ya Azam FC katika michuano ya kombe la Mapinduzi.

Azam FC walianza kwa kusuasua lakini sasa wanaonekana kuimarika vyema idara zao zote . Ni dhahiri michuano hii imewapa faida kubwa kutengeneza muunganiko mzuri wa uchezaji ( playing partnerships) na muunganiko kimbinu na kiufundi kwa ujumla pia saikolojia.

Safu ya ushambuliaji ya Azam FC inayoundwa na John Bocco , Yahya Mohamed na Joseph Mahudi upande wa kushoto imekuwa moto wa kuotea mbali . Ni dhahiri mwalimu Idd Nassoro Cheche amefanikiwa kuitengeneza pacha ya Yahya Mohamedi na John Bocco . Backline ya Simba SC hususani walinzi wa kati Method Mwanjale na Abdi Banda wanatakiwa kujiandaa vyema kuwazuia washambuliaji hawa ambao wana mudu mpira wa kasi kwa back up nzuri ya viungo nyuma yao Sure boy na Frank Domayo . Wote ni warefu kuicheza mipira ya juu .

Ukiwaacha Bocco na Yahya , Joseph Mahundi anaechezeshwa wing ya kushoto ameanza kuaminikia katika kikosi cha matajiri hao wa Chamazi . Mahundi ana kasi , uwezo mzuri wa kukokota mipira na kuachia mashuti ya mbali . Anacheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni ( winga ) . Janvier Bokungu ajiandae kwa ukinzani huu . Hii inaweza isimfanye akawa na wakati mzuri wa kupanda juu kusaidia mashambulizi na muda mwingi kubaki chini kusaidia marking .

Frank Domayo , Salumu Abubakari na Stephani ; wanaelewana vyema eneo la kiungo . Jonasi Mkude na James Kotei wajiandae kwa vita kubwa eneo hilo. Domayo amerudi vyema kwenye kiwango chake kama kiungo mkabaji . Anafanya vyema kwenye blocking,  pia kuanzisha mashambulizi kwa pasi zake nzuri ndefu na fupi . Si mgeni kwa viungo wa Simba na washambuliaji wake , anawajua vyema na ni mzoefu . Kazi ya kwanza ni kuvunja mawasiliano yao pale kati kisha kusaidia marking na kuiunganisha timu toka nyuma kwenda mbele . Wanaelewana vyema na Stephan ambaye hupangwa sambamba naye na yeye kupanda juu . Uwezo wa kupiga mshuti ni threat nyingine kwa Simba SC.

All in all ni mechi nzuri kushuhudia vita ya viungo , mpira wa kasi muda wote kwa aina ya uchezaji wa timu zote . Simba wazuri kuweka mpira chini kama ilivyo kwa Azam ingawa Azam sometimes hutumia mipira mirefu kumchezesha Bocco.

Uwezo wa fullbacks zake Gadiel na Kapombe kupandisha mashambulizi ni mtaji mwingine wa mashambulizi kwa Azam katika mechi ya kesho.

MROMANIA KOCHA MPYA AZAM FC

Mromania Kocha Mpya Azam FC

By Abducado Emmanuel on January 10, 2017

Category: First Team
Team: Azam FC
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.

Cioaba, 45, anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.

Kocha huyo atasaidiana na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na Kocha wa Makipa Idd Abubakar, walioiongoza timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo saa 10.15 jioni ya leo itasaka fainali kwa kukipiga na Taifa ya Jang’ombe.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, tayari wamefanikiwa kumpata kocha huyo na wameingia naye mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa.

Alisema Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika.

“Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC inapenda wadau wote wa mpira na wapenzi na mashabiki wa Azam kwamba klabu imempata mwalimu, ambaye ndiye ataiongoza klabu kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu.

“Kwa hiyo kwa mashabiki wetu maana yake ni kwamba tukiingia kwenye mechi inayofuata ya ligi, kocha atakuwa ameanza kazi na Cheche (Idd Nassor) atakuwa msaidizi wake na benchi lake zima alilokuwa nalo hivi sasa litaendelea,” alisema.

Kawemba aliongeza kuwa hivi sasa kocha huyo atakuwa na kikosi visiwani Zanzibar kufuatilia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri panapohitajika na ataanza rasmi kukaa kwenye benchi mpaka pale vibali vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika.

“Taratibu hizo zitakwenda kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo tutaziheshimu na kuona ya kwamba tutazifanya kwa haraka zaidi ili mwalimu aweze kupata kibali cha kufanya kazi hapa nchini, kwa hayo machache tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu wampe sapoti kocha na wadau wote wa mpira waone ya kwamba tumefanya jambo la kheri,” alisema.

Kauli ya kwanza ya Cioaba

Kwa upande wake Cioaba, alisema kuwa anafuraha kubwa leo hii kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi kazi nzuri na kuifanya timu hiyo kuwa bora.

“Najua Azam FC hapa Tanzania ni moja ya timu kubwa yenye historia huko nyuma, napenda kuushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa nafasi kuja kufundisha soka kwenye nchi hii, kwa mashabiki napenda kuwaambia kuwa nalijua soka la Afrika, nimewahi kufundisha Ghana na kupata matokeo mazuri.

“Kuhusu wakati ujao, nina furaha sana kuhusu uongozi walipoongea na mimi wakati tunaweka mipango ya timu ya hapo baadaye na hili ni jambo zuri kwa kocha, kitaaluma nawaahidi mashabiki na watu wote wanaoipenda Azam FC, niko hapa kuwapa mambo mazuri katika kazi yangu kwenye klabu,” alisema.

Msimu uliopita, Cioaba aliiongoza Aduana Stars ya Ghana kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Ghana, ambapo anafahamiana kwa ukaribu na nyota wawili wa Azam FC, Yakubu Mohammed na Yahaya Mohammed, waliosajiliwa kutoka timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.

Mbali na kufundisha soka nchini Ghana pia amewahi kufanya kazi kwenye miamba ya Morocco, Raja Casablanca, Al Masry ya Misri na katika nchi za Romania, Kuwait, Oman na Jordan.

Ratiba Africon 2017

Supersport.com
*AFCON 2017 FIXTURE*

14 January 2017 14 Jan 18:00
Gabon v Guinea-Bissau

14 January 2017 14 Jan 21:00
Burkina Faso v Cameroon

15 January 2017 15 Jan 18:00
Algeria v Zimbabwe

15 January 2017 15 Jan 21:00
Tunisia v Senegal

16 January 2017 16 Jan 18:00
Cote d'Ivoire v Togo

16 January 2017 16 Jan 21:00
DR Congo v Morocco

17 January 2017 17 Jan 18:00
Ghana v Uganda

17 January 2017 17 Jan 21:00
Mali v Egypt

18 January 2017 18 Jan 18:00
Gabon v Burkina Faso

18 January 2017 18 Jan 21:00
Cameroon v Guinea-Bissau

19 January 2017 19 Jan 18:00
Algeria v Tunisia

19 January 2017 19 Jan 21:00
Senegal v Zimbabwe

20 January 2017 20 Jan 18:00
Cote d'Ivoire v DR Congo

20 January 2017 20 Jan 21:00
Morocco v Togo

21 January 2017 21 Jan 18:00
Ghana v Mali

21 January 2017 21 Jan 21:00
Egypt v Uganda

22 January 2017 22 Jan 21:00
Guinea-Bissau v Burkina Faso

22 January 2017 22 Jan 21:00
Cameroon v Gabon

23 January 2017 23 Jan 21:00
Senegal v Algeria

23 January 2017 23 Jan 21:00
Zimbabwe v Tunisia

24 January 2017 24 Jan 21:00
Togo v DR Congo

24 January 2017 24 Jan 21:00
Morocco v Cote d'Ivoire

25 January 2017 25 Jan 21:00
Egypt v Ghana

25 January 2017 25 Jan 21:00
Uganda v Mali