Simba SC wajipange vyema mechi ya kesho dhidi ya Azam FC katika michuano ya kombe la Mapinduzi.
Azam FC walianza kwa kusuasua lakini sasa wanaonekana kuimarika vyema idara zao zote . Ni dhahiri michuano hii imewapa faida kubwa kutengeneza muunganiko mzuri wa uchezaji ( playing partnerships) na muunganiko kimbinu na kiufundi kwa ujumla pia saikolojia.
Safu ya ushambuliaji ya Azam FC inayoundwa na John Bocco , Yahya Mohamed na Joseph Mahudi upande wa kushoto imekuwa moto wa kuotea mbali . Ni dhahiri mwalimu Idd Nassoro Cheche amefanikiwa kuitengeneza pacha ya Yahya Mohamedi na John Bocco . Backline ya Simba SC hususani walinzi wa kati Method Mwanjale na Abdi Banda wanatakiwa kujiandaa vyema kuwazuia washambuliaji hawa ambao wana mudu mpira wa kasi kwa back up nzuri ya viungo nyuma yao Sure boy na Frank Domayo . Wote ni warefu kuicheza mipira ya juu .
Ukiwaacha Bocco na Yahya , Joseph Mahundi anaechezeshwa wing ya kushoto ameanza kuaminikia katika kikosi cha matajiri hao wa Chamazi . Mahundi ana kasi , uwezo mzuri wa kukokota mipira na kuachia mashuti ya mbali . Anacheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni ( winga ) . Janvier Bokungu ajiandae kwa ukinzani huu . Hii inaweza isimfanye akawa na wakati mzuri wa kupanda juu kusaidia mashambulizi na muda mwingi kubaki chini kusaidia marking .
Frank Domayo , Salumu Abubakari na Stephani ; wanaelewana vyema eneo la kiungo . Jonasi Mkude na James Kotei wajiandae kwa vita kubwa eneo hilo. Domayo amerudi vyema kwenye kiwango chake kama kiungo mkabaji . Anafanya vyema kwenye blocking, pia kuanzisha mashambulizi kwa pasi zake nzuri ndefu na fupi . Si mgeni kwa viungo wa Simba na washambuliaji wake , anawajua vyema na ni mzoefu . Kazi ya kwanza ni kuvunja mawasiliano yao pale kati kisha kusaidia marking na kuiunganisha timu toka nyuma kwenda mbele . Wanaelewana vyema na Stephan ambaye hupangwa sambamba naye na yeye kupanda juu . Uwezo wa kupiga mshuti ni threat nyingine kwa Simba SC.
All in all ni mechi nzuri kushuhudia vita ya viungo , mpira wa kasi muda wote kwa aina ya uchezaji wa timu zote . Simba wazuri kuweka mpira chini kama ilivyo kwa Azam ingawa Azam sometimes hutumia mipira mirefu kumchezesha Bocco.
Uwezo wa fullbacks zake Gadiel na Kapombe kupandisha mashambulizi ni mtaji mwingine wa mashambulizi kwa Azam katika mechi ya kesho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni